Khaji Mzaro (17), mkazi wa Manzese jijini Dar, yupo katika wakati mgumu baada ya mguu wake wa kushoto kuvimba na kumfanya kukatisha masomo yake na kuendelea kujiuguza pasipo kujua hatima ya maisha yake.
Khaji Mzaro akiwa na maumivu makali baada ya kuvimba mguu.
Hali ilivyoanza
Akizungumza na waandishi wetu kwa simanzi kijana huyo alisema, alizaliwa akiwa mzima na mwaka jana mguu huo ulianza kuvimba taratibu katika eneo la kisigino.Akifafanua zaidi alisema: “Pasipo kujua tatizo ni nini wazazi wangu wakaamini kwamba inawezekana kuna mtu ‘kanichezea’ kishirikina kijijini kwetu.
“Huu ni ugonjwa wa ajabu kwangu, siku moja niliamka nikakuta ghafla mguu wangu umevimba na wakati unaanza ‘kujaa’ nilikuwa najisikia kuchoka tu lakini ulikuwa hauumi kabisa.“Kuna wakati nikikaa ndani tu bila kutoka kwenda kokote uvimbe unapungua lakini nachoka kukaa, hapo ndipo wazazi wakaona kuna namna.
NASIKITIKA KUTOKWENDA SHULE
“Mimi huwa napenda niwe natembeatembea angalau ninyooshe miguu, nikionana na vijana wenzangu huko nje huwa nafarijika sana japo sina uwezo wa kucheza mpira kama zamani au kwenda shule. “Naumia sana kuona masomo yananipita kila siku nikiamka hali yangu ni hii siwezi kwenda shule, najisikia vibaya nikiwaona watoto wenzangu wanapita wakiwa wanatoka shule, napenda sana kusoma ili niwe na maisha mazuri baadaye.”
Wamezunguka hospitali bila mafanikio
Bibi wa kijana huyo, Caroline Francis alielezea jinsi walivyozunguka hospitali mbalimbali bila mafanikio na ndipo wakaamua kwenda kwa waganga wa kienyeji ambao nao wamegonga mwamba.
“Kwa kweli tumehangaika sana mpaka sasa tumekata tamaa na fedha zimetuishia. Bado tunajitahidi kwenda kliniki kila mwezi kwa ajili ya vipimo huku tukisubiri madaktari bingwa kutoka India.
Muonekano wa mguu uliovimba.
BIBI YAKE AFUNGUKA
“Tangu uvimbe ulipomuanza akiwa darasa la nne mwaka jana mwezi wa tano akiwa Kondoa kwa wazazi wake na kumsababishia aache shule, hajapata raha, tukaamua aje hapa Dar kwa ajili ya matibabu.“Tuliamua aje huku kwa sababu Kondoa alitibiwa hospitali na pia wazazi wake baada ya kuona hakuna mafanikio, walijaribu kumpeleka kwa waganga mbalimbali kwa kuamini amerogwa akawa anapata afuweni kwa kipindi kifupi na hali kurejea tena baada ya muda fulani.
“Inasikitisha, mpaka sasa hivi mguu wake kama unavyoonekana huwa unavimba sana na huwa analalamika kwa kuwa unamuuma sana.”“Hivi sasa ikabidi tuelekeze nguvu zetu hospitali tumefika mpaka Hospitali ya Muhimbi Moi tukaambiwa kuwa tatizo lipo kwenye mishipa yake ya sehemu hiyo yenye uvimbe.
KUWEKEWA MISHIPA YA PLASTIKI
“Madaktari wamesema kuna mishipa imepishana hivyo anatakiwa apasuliwe ili awekewe mishipa ya plastiki lakini hawakutuambia gharama ni kiasi gani tunajua lazima gharama itakuwa kubwa japokuwa sasa anatumia dawa mbalimbali bado hatuoni akipata nafuu.”Kwa yeyote aliyeguswa na stori hii anaweza kumsaidia kijana Khaji kwa kupitia namba 0786 536 692, 0719 024 088.
0 comments:
Post a Comment