2014-12-17

Haiti waandamana kumng'oa Rais wao

Rais wa Hait: Michael Martelly


Mamia ya raia wa nchini Haiti wameandamana katika mitaa ya Port-au-Prince wakishinikiza Rais Michel Martelly kuondoka madarakani.

Hata hivyo maandamano hayo yamegeuka vurugu baada polisi kutumia mabomu ya mchozi kuwatawanya waandamanaji hao. polisi wamepambana na waaandamanaji hao ambao wamekuwa wakirusha mawe na kuchoma moto matairi mitaani.

Madai ya raia hao ni kumtaka Rais Martelly kuitisha uchaguzi na kuunda serikali,ambapo uchaguzi ulitakiwa kuitishwa miaka mitatu iliyopita.

Waziri mkuu wa Haiti Laurent Lamothe, siku ya jumapili aliamua kuachia ngazi baada ya shinikizo la siku mbili.Maoni kutoka vyama vya upinzani ni kwamba wanamtaka rais Martelly kujiuzulu. Awali Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry ameitaka Hait kuitisha uchaguzi mara moja.

BBC


0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...