2014-12-22

HAYA SASA; JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

images
AITWAYE JOHN EMANUEL (36) MKAZI WWATU TISA [09] KATI YAO WANAUME SABA [07] NA WANAWAKE WAWILI [02] WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA GARI WALIOKUWA WAKISAFIRIA LENYE NAMBA ZA USAJILI T.203 ARZ AINA YA TOYOTA COASTER LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA. 


A MLOWO-MBOZI LIKIWA LINATOKEA MBEYA KWENDA TUNDUMA WAKATI AKIJARIBU KULIPITA GARI T.789 AZL/T.123 AXV AINA YA TATA TRUCK ENEO AMBALO KUNA MLIMA NA MBELE YAKE KUNA KONA LILITOKEA GARI T.903 CVF AINA YA TATA BASI HIVYO DEREVA WA COASTER KULAZIMIKA KUINGIA MBELE YA LORI ALILOKUWA ANALIPITA NA KUGONGWA UBAVUNI UPANDE WA KUSHOTO PIA KUGONGWA UPANDE WA KULIA NA BASI AINA YA TATA TAJWA HAPO JUU. 


TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 21.12.2014 MAJIRA YA SAA 14:10 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA CHENGULA, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA, BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA. MAREHEMU WALIOTAMBULIKA KWA MAJINA NI WANNE AMBAO NI 1. THOMAS SIMFUKWE (35) 2. EXAVERY MUMBISA (34) 3. AMINA MAIKO (30) 4. NEEMA ALMASI 5. HEBELI MKILIMI 6. ROSE HEZRON HALELE NA 7. ALIYEFAHAMIKA KWA JINA MOJA JANUARI. 

HATA HIVYO MIILI YA MAREHEMU WATATU BADO KUTAMBULIWA. AIDHA KATIKA AJALI HIYO WATU KUMI NA MOJA [11] WALIJERUHIWA AMBAO MAJERUHI SITA [06] WANAUME, WANNE [04] WANAWAKE, WAWILI WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA AMBAO NI DEREVA AITWAYE JOHN EMMANUEL MZUMBA (36) MKAZI WA MLOWO NA KONDAKTA AITWAYE CHRISTIAN MTENDE (31) MKAZI WA MLOWO NA WENGINE SABA WALIPELEKWA KATIKA HOSPITALI YA SERIKALI WILAYA YA MBOZI NA KITUO CHA AFYA TUNDUMA KWA MATIBABU.
CHANZO CHA AJALI NI UZEMBE WA DEREVA WA TOYOTA COASTER KUTAKA KUYAPITA MAGARI YALIYOKUWA MBELE YAKE BILA KUCHUKUA TAHADHARI.
KATIKA TUKIO LA PILI:
DEREVA WA LORI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA HAMAD AHMAD @ MASAWE (30) MKAZI WA DSM AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA GARI ALILOKUWA AKIENDESHA LENYE NAMBA ZA USAJILI T.769 ARX AINA YA SCANIA KUACHA NJIA NA KUPINDUKA ENEO LA SENJELE WILAYA YA MBOZI.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 21.12.2014 MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI CHA SENJELE, KATA YA RUANDA, TARAFA YA IYULA, WILAYA YA MBOZI, BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA, MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHUIWA HASPITALI YA SERIKALI YA WILAYA YA MBOZI. 

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA.
KATIKA TUKIO LA TATU: 

MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA 08 ALIYETAMBULIKA KWA JINA SHIMBI MWANDU MKAZI WA KIJIJI CHA MKUNYWA ALIKUTWA AMEKUFA MAJI KATIKA MFEREJI UNAOPELEKA MAJI KATIKA MASHAMBA YA MPUNGA WILAYANI MBARALI
MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA KATIKA MFEREJI HUO MNAMO TAREHE 21.12.2014 MAJIRA YA SAA 09:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MLONGA, KIJIJI CHA MKUNYWA, KATA YA MADIBIRA, TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. 

UCHUNGUZI WA AWALI UNAONYESHA KUWA MAREHEMU ALIKUNYWA MAJI MENGI NA KUKOSA HEWA AKIWA NDANI YA MAJI YA MFEREJI HUO HALI ILIYOPELEKEA KIFO CHAKE. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWA MAKINI NA WATOTO WAO HASA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA KWA KUWEKA UANGALIZI WA KUTOSHA. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUFUNIKA VISIMA, KUFUKIA MASHIMO NA MITARO KWANI NI HATARI KWA WATOTO.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...