Aisha Madinda Enziza uhai wake.
Amekwenda mapema mno! Siku ya Desemba 17, mwaka huu haikuwa poa hata kidogo kwenye tasnia ya muziki wa dansi Bongo katika kipengele cha unenguaji.
Chumba chetu cha habari kinachofanya kazi kwa karibu na mastaa Bongo kilipata mshtuko wa aina yake.
Zilikuwa ni habari mbaya za kifo cha aliyekuwa mnenguaji bei mbaya wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’ inayosimamiwa na Kampuni ya ASET chini ya mkurugenzi wake, Asha Baraka, Mwanaisha Mohamed Mbegu. Wengi tulimzoea kwa jina la stejini la Aisha Madinda.
&n
AZALIWA OCEAN ROAD
AZALIWA OCEAN ROAD
Katika mahojiano aliyofanya na magazeti yetu kwa nyakati tofauti, kabla ya kujiingiza kwenye sanaa ya unenguaji na baada ya kuugua kwa muda mrefu kisha kupona na kukutwa na umauti, Aisha alieleza kwamba alizaliwa jijini Dar katika Hospitali ya Ocean Road.
Aisha Madinda akiwa na mkurugenzi wa ASET Asha Baraka. Hiyo ilikuwa Mei 5, 1979.
Hivyo ameondoka mapema akiwa na umri wa miaka 35 tu. Baada ya maisha ya utoto, Aisha alipelekwa mkoani Kigoma ambako ndiko alikokulia.
0 comments:
Post a Comment