2014-12-19

NI KITIMTIM:BUNGENI KENYA! NAIBU SPIKA WA BUNGE AMWAGIWA SODA!


Naibu spika Joyce Laboso pichani ambaye amemwagiwa soda

Kikao cha adhuhuri cha wabunge nchini Kenya, kinaendelea kuzua hisia kali hukuwabunge wakiendelea kuvurugana humo.
Wabunge hao wanajadili mswada tatanishi wa usalama ambao upande wa upinzani unasema unakwenda kinyume na katiba na kuwanyima wakenya haki yao ya kujieleza. 
                                  

Mmoja wa wabunge hao wa upinzani amemwagia soda naibu spika Joyce Laboso ambaye alikuwa anasimamia kikao hicho cha kufanyia mswada huo mabadiliko kabla ya kupitishwa.

Spika wa bunge hilo sasa amechukua usukani na kuamuru kutimuliwa kwa wabunge wawili waliokuwa wamezidi vurugu.
 

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...