2014-12-17

Kaka wa rais wa zamani wa Mexico afutiwa mashitaka ya utajiri haramu

Jaji wa mahakama ya shirikisho nchini Mexico imemfutia mashitaka yote ya kujipatia utajiri kinyume cha sheria kaka wa rais wa zamani wa nchi hiyo, Carlos Salinas.
 Afisa mmoja wa mahakama huyo aliyezungumza kwa masharti ya kutotajwa jina, amesema mashitaka ya mwisho dhidi ya Raul Salinas, yalifutwa wiki iliyopita, lakini bado hayajatangazwa.
                               
 Afisa huyo hakutoa sababu za kufutwa kwa mashitaka hayo. Salinas alishatumikia kifungo cha miaka 10 gerezani kwa mauaji ya shemegi yake wa kiume mwaka 1994, wakati akiwa mtu wa pili kwa umuhimu kwenye Chama Tawala cha Taasisi ya Mapinduzi. 
                                    
Alifutiwa tuhuma za mauaji hayo mwaka 2005, na pia mashitaka mengine ya kutakatisha fedha haramu, ingawa wachunguzi waligundua kiasi cha dola milioni 100 kwenye akaunti zake za benki nchini Uswisi, zinazokisiwa kupatikana baina ya mwaka 1988 na 1994, wakati kaka yake akiwa rais

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...