ALIYEKUWA memba wa kundi la Chamber Squad, Moses Bushagama ‘Mez B’ ambaye alifariki Ijumaa iliyopita mjini Dodoma anatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Wahanga yaliopo Maili Mbili mjini Dodoma.
Mama Mzazi wa aliyekuwa Msanii wa Kizazi Kipya Marehemu Mez B ameelezea Sababu ya Kifo cha Mez B kwamba ni Ugonjwa wa Pneumonia ambao ulikuwa unamumbua siku nyingi.
Katika Taarifa ya Mama Mzazi wa Mez B amesema kuwa Mez B alilazwa na Kuruhusiwa Mara Kadhaa katika Hospitali ya Mwananchi Dodoma na Juzi juzi Alilazwa kwa takribani Siku 8 na baadae Aliruhusiwa na Madaktari wakampa moyo kuwa Atarudi katika hali yake ya Kawaida.
0 comments:
Post a Comment