2014-12-17

Ni balaa:Bush mwengine ataka urais wa Marekani

 
 Gavana wa zamani wa jimbo la Florida nchini Marekani Jeb Bush amesema anataka kujitosa katika kinyang’anyiro cha Uraia wa Marekani uchaguzi mkuu wa 2016.


Gavana wa zamani wa Florida, Jeb Bush, amesema anafikiria uwezekano wa kugombea urais wa Marekani hapo mwakani.
 Jeb ni kaka wa George Walker Bush aliyekuwa rais wa nchi hiyo kutoka mwaka 2001 hadi 2009. 
Baba yao, George Herbert Bush aliiongoza Marekani kutoka mwaka 1989 hadi 1993.
                                  
 Ikiwa Jeb ataamua rasmi kugombea, anatazamiwa kupata uungaji mkono mkubwa wa mtandao wa kisiasa wa familia yake na kuvutia ufadhili wa matajiri wakubwa ambao kawaida hutumiwa na chama cha Republican kuchangia kampeni zake.
                                 
 Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na pia mke wa rais wa zamani, Hillary Clinton, kwa sasa ndiye anayeangaliwa kuwa mgombea wa chama cha Democrat cha Rais Barack Obama.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...