Watu wawili kati ya wanne wanaosadikiwa kuwa majambazi wameuawa na wananchi wenye hasira baada ya jaribio lao la kutaka kupora fedha zaidi ya shilingi milioni 100.
Watu wawili kati ya wanne wanaosadikiwa kuwa majambazi wameuawa na wananchi wenye hasira baada ya jaribio lao la kutaka kupora fedha zaidi ya shilingi milioni 100 katika kiwanda cha kutengeneza chokaa cha Nelkanth kilichopo eneo la Amboni jijini Tanga kushindikana.
/span>
Kaimu kamanda wa polisi mkoani Tanga kamishina msaidizi wa polisi Juma Ndaki amewataja majambazi waliouawa kuwa ni Timoth Charles mkazi wa Mkwajuni jijini Dar es Salaam na mwinyimkuu Hamisi mkazi wa mtaa wa chanika ambao walikuwa wakitumia usafiri wa pikipiki aina ya boxer huku wenzao wawili wakikimbia kusikojulikana.
 
k
0 comments:
Post a Comment