2014-12-22

MAMBO YA KRISMAS MKE WA MTU ANASWA AKIJIUZA KUSAKA FEDHA ZA KRISMASI



Makamanda wa Polisi pamoja na kikosi cha OFM wakiwataiti wanawke waliokuwa wakijiuza.Ni aibu iliyoje! Tabia ya wanawake kujiuza kwa kisingizio cha kusaka fedha kwa ajili ya Sikukuu ya Krismasi imewatokea puani wanawake zaidi ya kumi akiwemo mke wa mtu baada ya kunaswa mawindoni na kutiwa nguvuni. 



Tukio hilo la aibu lilitokea katika msako maalum wa polisi waliotoa kolabo kwa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers, uliofanyika katika eneo ‘korofi’ la ltinga, Msamvu Kata ya Mwembesongo mkoani hapa, wikiendi iliyopita.
Wanawake hao wakiwa chini ya ulinzi mkali. Awali, Kamanda wa OFM mkoani hapa alipokea malalamiko lukuki kutoka kwa wananchi waishio jirani na eneo hilo waliokuwa wakiwalalamikia wanawake hao kugeuza vibanda vyao vya simu kuwa gesti na kuvitumia kufanyia ngono usiku na kuzagaa kwa kondom kila sehemu

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...