Baadhi ya waliookolewa kutoka ndani ya mgahawa wa Lindt
Polisi nchini Australia wanasema kuwa wanafanya mazungumzo na mwanamme moja aliye na silaha saa kadhaa baada ya kuwateka nyara watu kadha kwenye mgahawa mmoja katikakati mwa mji wa Sydeney.
Mamia ya polisi waliojihami vikali wamezingira jengo hilo .
Police wanasema kuwa wamewasiliana na jamaa mmoja aliyejihami na ambaye anawazuilia watu ndani ya mgahawa huo.
Takriban watu watatu wameonekana ndani ya mgahawa wakiwa wamenyanyua mikono juu wakiwa wameiegesha kwenye dirisha wakiwa wameshika bendera nyeusi ikiwa na maandishi ya kiarabu.
Katika hotuba yake kwa taifa, Waziri mkuu Australia Tony Abbott, amesema kuwa serikali inafanya kila liwezalo kuwanusuru watu hao.
Mmoja wa waliokuwa ndani ya mgahawa ambao uliovamiwa na watekaji nyara mjini Sydney
Waziri Mkuu wa Australia Tony Abbot amesema tukio hilo linahuzunisha sana.
Abbot amesema haijajulikana nani amehusika na tukio hilo hata hivyo anahisi huenda ni njama za kisiasa na kuwa tayari kamati ya usalama ya taifa imepewa taarifa.
Kamishna wa Polisi wa South Wales Andrew Scipione amesema tukio hilo halichukuliwi kuwa la kigaidi lakini imethibitishwa kuwa kuna mtu mwenye silaha anayewashikilia mateka watu kadhaa.
Mashahidi wa tukio hilo wamesema walimuona mtu akiwa na begi na silaha akiingia kwenye mgahawa, polisi wamefunga eneo hilo, barabara na kuwaondoa watu katika eneo hilo.
Polisi nchini Australia wakiwa wameuzingira mgahawa uliovamiwa na mtu aliyejihami na kuwateka nyara watu kadhaa
Polisi wanaonya kuwa wavamizi hao huenda wakaendelea kuwazuilia raia hao kwa zaidi ya siku moja.
Watu watano walikimbilia usalama wao huku wakionekana kupata afueni walipowafikia polisi hao.
Haijulikani ikiwa walitoroka kutoka mikononi mwa wavamizi au vinginevyo.
Polisi wanasema kuwa wana taarifa kuhusu watekaji nyara hao.
Hawajaweza kuthibitisha ikiwa wammepewa matakwa yoyote kutoka kwa mtekaji nyara huyo kupitia miatndao ya kijamii.
Bendera nyeusi inayofanana na ile ya kundi la wapiganaji wa kiisilamu la IS yenye maandiko ya kiarabu, imekuwa ikipeperushwa kwenye dirisha la mgawaha huo, huku waziri mkuu Tony Abbott,akisema huenda uivamizi huu umeshinikizwa kisiasa
0 comments:
Post a Comment