2014-12-15

WADHIHIRISHA SI KILA MBRAZIL ANAJUA KUCHEZA MPIRA…KIIZA BADO ‘KIDUMEJAJA, COUTINHO, EMERSON





YANGA SC wamekuwa wateja wa Simba katika mechi mbili za ‘Nani Mtani Jembe’. 

Desemba 21 mwaka jana walifungwa mabao 3-1 na Mnyama Simba na jana walitandikwa mabao 2-0.
Katika mechi ya jana, wachezaji wa kigeni wa Yanga walikuwa Emerson Oliveira, Andrey Coutinho, Kpah Sherman, Mbuyu Twite na Haruna Niyonzima. 

Hamis Friday Kiiza tayari walishamtoa, lakini cha kuwashauri Yanga ni kufanya kila wawezalo kumbakisha Mganda huyu kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa kesho. 

Kiiza bado ana mkataba na Yanga, wamchukue na kuwakata Wabrizil wote wawili, Emerson na Coutinho, halafu watafute mchezaji mwingine. 

Itakuwa jambo zuri akibaki Kiiza ili acheze na Sherman kwasababu wale Wabrazil hawana kitu.
Kiiza ni mchezaji ambaye hajawahi kuiangusha Yanga, ila kinachomgharimu ni misimamo yake ya kutaka kutetea haki zake. 

Utakuta amekubaliana na viongozi wa Yanga kumsajili kwa milioni 20, lakini wanataka kumpa milioni 10. Yeye anakuwa mbishi, anagoma kumkopa na hapo ndipo anaonekana mtovu wa nidhamu. 

Kama viongozi wanamtoa kwasababu ya kutetea maslahi yake wanajikomoa wenyewe.
Kiiza katika mechi kubwa kama ya jana huwa ni mchezaji wa kiwango chaa juu, hakuna mchezaji anayecheza kwa kiwango cha juu kama Kiiza. 
 

Kiiza hajawahi kuiangusha Yanga, lakini alivyokuja Maximo alimtengenezea mazingira ya kuonekana hafai ili kumpa nafasi Jaja.
Kweli Kiiza kavumilia, Jaja ameshindwa na kukimbia, halafu wamemsajili Kpah Sherman, Daniel ‘Danny’ Davis Mrwanda ambao ni wazuri, lakini kwa Emerson imekula kwao.

Licha ya usajili huo, bado Kiiza ndio mwokozi wa Yanga.Wasione dhambi kula matapishi yao, wasiogope kurudi nyuma kwani ndio uanaume. Mwanaume akigundua amekosea, anarudi nyuma kurekebisha ili maisha yaendelee.
Yanga warudi kwa Kiiza, wawakate Wabrazil, Kiiza bado ni mchezaji wa Yanga. 

Mechi ya jana kama Kiiza angekuwepo halafu akacheza na Sherman, Yanga wangeweza kuisumbua Simba SC.
Sherman ana nguvu, uwezo wa kumiliki mpira, hivyo alikuwa anahitaji mtu mwingine muelewa kama Kiiza. 

Kiiza ana akili ya mpira, anajua namna ya kujipanga. Yanga watatengeneza timu nzuri kwa uwepo wa Sherman na Kiiza. Hakika watasahau mapungufu yao yote.
Ermeson na Coutinho wapigwe panga, mechi ya jana iwe ya mwisho kwao, mimi nitashangaa sana nikiona wanaendelea kuwepo wakati hawana uwezo. 

Nafasi ya Emerson acheze Salum Telela, Mbrazil gani anakuja kufanya majaribio?
Mimi na watu wengi tuliamini kuwa kila Mbrazil anajua kucheza mpira kutokana na historia ya nchi hiyo, kumbe sio kila Mbrazl anajua kucheza mpira. Hii imethibitishwa na akina JaJa, Coutinho na Emerson.
Yanga ni ile ile, wachezaji ni walewale, Maximo na Wabrazil ndio walioivuruga timu.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...