Rais wa Simba SC Evans Aveva atakutana na waandishi wa habari jijini hapa kesho kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu klabu hiyo ya Msimbazi.
Aveva anayetoka Kundi la Matajiri wa Simba (FoS), aliahidi kuzungumza na waandishi wa habari kwa kina juu ya suala linalotajwa la Simba Ukawa wanaohusishwa na matokeoa mabaya ya timu hiyo iliyoifunga Yanga SC Jumamosi.
Hamphrey Nyasio, Msemaji wa Simba SC, amesema jioni hii kwamba Rais huyo atavunja ukimya juu ya Simba Ukawa na masuala mengine mengi yanayoihusu klabu hiyo.
Simba imekuwa na mwanzo mbaya katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu huu ikitoka sare katika michezo sita ya awali kabla ya kushinda 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mechi yao ya raundi ya saba.
Wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Simba SC, Aveva alikuwa na sera ya vidole vitatu kila mkono akimaanisha kila mechi pointi tatu na magoli matatu lakini sera hiyo inaonekana kufeli katika mechi zote zilizopita tangu aingie madarakani kwani Simba haijawahi kuonja ushindi huo .
0 comments:
Post a Comment