Dar es Salaam. Kocha mkuu wa Kagera Sugar, Jackson Mayanja amesema anaihofia zaidi Yanga na si Simba atakayocheza nayo Jumapili ijayo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mayanja alisema kuondoka kwa Amissi Tambwe kwenye kikosi cha Mzambia Patrick Phiri kumempa ahueni na sasa haihofii timu hiyo kwa mchezo wao wa Jumapili.
Mayanja alisema kuondoka kwa Amissi Tambwe kwenye kikosi cha Mzambia Patrick Phiri kumempa ahueni na sasa haihofii timu hiyo kwa mchezo wao wa Jumapili.
“Tambwe alikuwa mfungaji kila tulipocheza nao. Kila alipokuwapo uwanjani sikuwa na amani. Kuondoka kwake Simba kumeipunguza presha timu yangu kwenye mechi yetu ya Jumapili na sasa siihofii sana Simba kama ambavyo nitakuwa na presha tukicheza na Yanga kwani ni lazima niwe na tahadhari zaidi na Tambwe,” alisema Mayanja.
Alisema wameamua kuja Dar es Salaam mapema ili kuzoea mazingira na hali ya hewa ya jiji ambayo ni ya joto kabla ya mechi hiyo na kusisitiza kuwa anaiheshimu Simba kutokana na kufanya usajili bora sasa.
“Simba ni timu nzuri, ina mashabiki wengi na kipindi hiki imefanya usajili zaidi yetu. Najua mechi itakuwa ngumu, lakini mwamuzi akifuata sheria zote mashabiki wataona soka safi na bila shaka Kagera itaondoka na ushindi,” alisema Mayanja.
Alisema licha ya majeruhi wawili alionao kwenye timu yake, wachezaji wengine wako tayari kupambana na kusisitiza kuwa Kagera haichezi mpira wa maonyesho bali kupambana na kupata pointi tatu.
0 comments:
Post a Comment