2015-03-23

MVUA YAGEUKA KERO KUBWA KWA WAKAZI WA DAR

Soko la Mchikichini, Ilala-Boma linavyoonekana kufuatia mvua za sasa
Maji yalivyotapakaa soka la Sinza Afrika-Sana. 


Wakazi wa Mwanayamala-Mkwajuni wakitoa maji katika nyumba zao. 

...Juhudi za kuondoa maji zikiendelea. 



Mwonekano wa nyumba za bonde la Mchikichini, Ilala-Boma.

WAKATI mvua zikiendela kunyesha katika jiji la Dar es Salaam, na sehemu nyingine nchini, wakazi wake wengi wameonekana kuhangaika kupata sehemu salama za kuishi na kufanyia biashara.

Mtandao huu umezungukia maeneo mbalimbali ya jiji na kukuta wakazi wa maeneo mengi wakitoa maji kwenye nyumba zao na sehemu za kufanyia biashara.

Wakiongea na mwandishi wetu, wakazi wa maeneo ya Mwanayamala-Mkwajuni maarufu kama Bondeni, wameitupia lawama kampuni ya ujenzi ya Strabag kuwa imechangia nyumba zao kuingiliwa na maji kwani mifereji iliyotengenezwa haikidhi uwezo wa kusafirisha maji kwa kasi kwani ni midogo na badala yake maji hujaa na kuelekea katika makazi yao. 

Katika maeneo ya Jangwani mtandao huu ulikuta baadhi ya nyumba zilizoko bondeni zikiwa karibu kumezwa na maji, ambapo wakazi wa maeneo hayo wametaka serikali iwasaidie.

Katika soko la Sinza Afrika-Sana, wafanyabiashara ndogondogo wa soko hilo wameelezea kero inayosababishwa na mifereji inayopitisha maji barabarani kuziba kufuatia uchafu unaotupwa ovyo na hivyo kuelekeza maji katika biashara zao na wateja kukosa sehemu ya kupita.

Vilevile, wafanyabiashara ndongondogo eneo la Ilala-Boma katika soko la Mchikichikini, wamesema mvua zinazoendelea zinawafanya wengi wao kukosa fedha ya kujikimu kutokana na wateja kutokufika kwenye vibanda vyao kwani maji yanajaa sehemu hizo zaq biashara. 


GPL

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...