MWIGIZAJI mahiri Riyama Ally, amesema baada ya kuigiza filamu nyingi za watu, safari hii ameamua kuonyesha upande wake wa pili baada ya kuandika muswada wa filamu yake mpya iitwayo ‘Msuto Daily’.
Riyama ameelezea filamu hiyo ambayo tayari imeshapelekwa sokoni, kuwa ni kazi ya mikono yake ambapo amejitahidi kuonyesha ubunifu kwa lengo la kushibisha soko lake.
“Msuto Daily ni kazi ya mikono yangu, nimetunga stori na kucheza kama mhusika mkuu. Ni filamu ya Kiswahili na imechezwa uswahilini haswaa, chezea vyumba sita wewe. Humu ndani umbea kwa kwenda mbele hasa ukiujulia maana umbea kipaji, mashabiki wanaweza kupata nakala zao sehemu wanazouza CD maana kazi ilishatoka,” alisema mwigizaji huyo.
0 comments:
Post a Comment