2014-12-15

Sikia alichosema Idris Sultan: "Sina mpango wa kubadilika"


“Sina sababu ya kubadilika baada ya kushinda na kupata fedha nitakachofanya ni kubadili mfumo wa zamani na kuwa wa sasa,” alisema Sultan. 

Mshindi wa shindano la Big Brother Afrika 2014, Idris Sultan amesema yeye ni wa kawaida na hana mpango wa kubadilika.
Akizungumza na Mwandishi wetu jijini Dar es Salaam, Sultan, alisema hana sababu ya kubadilika atakachokifanya ni kubadilisha staili aliyokuwa akiishi zamani.

“Sina sababu ya kubadilika baada ya kushinda na kupata fedha nitakachofanya ni kubadili mfumo wa zamani na kuwa wa sasa,” alisema Sultan.

Aidha, Sultan alisema anataka kufanya ‘komedi’ na kubadili mawazo ya vijana ambao baadhi yao hawako kwenye maadili mema. Alisema vijana hawapaswi kukata tama wanapodhamiria kufanya jambo lolote.

Alisema wanapoanza, waweke nia ya kufanikiwa wasikate tamaa. Suala la msingi ni kujiamini,” alisema.



0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...