Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Hawa Ghasia akiwaeleza waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mafanikio ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika jana kote nchini ambapo umefanikiwa kwa asilimia 98%, kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne Sagini.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh.Hawa Ghasia (hayupo pichani) na vyombo vya habari uliofanyika leo jijini Dar es salam ukilenga kueleza hatua zitakazochukuliwa na Serikali kwa wale wote waliosababisha kasoro mbalimbali katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika jana kote nchini.
Michuzi
0 comments:
Post a Comment