Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Servacius Likwelile mara baada ya kuwasili viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe jijini Dar es salaam ambapo linafanyika tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne mwishoni mwa wiki kuelekea maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Watumishi wa wizara ya Fedha na taasisi zake wakiwa kwenye maandamano ya tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne mwishoni mwa wiki kuelekea maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Servacius Likwelile akimkaribisha Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum kufungua tamasha siku nne (Disemba 6 hadi 7, 2014) la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne mwishoni mwa wiki kuelekea maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akifungua tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne mwishoni mwa wiki lililoandaliwa na Wizara ya Fedha kwa kuandaa mashindano ya fani ya sanaa za maonesho yanayofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Doroth Mwanyika wakati wa ufunguzi wa tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne linalofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akimkabidhi cheti maalum cha ushiriki Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano Serikalini (GCU) Ingiahedi Mduma wakati wa ufunguzi wa tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne linalofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe jijini Dar es salaam.
Afisa Uendeshaji PSPF Delphin Richard akikabidhiwa cheti maalum na Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum cha ushiriki wa tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne linalofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe jijini Dar es salaam.
Wanakwaya kutoka Wizara ya Fedha wakiimba wakati wa mashindano ya sanaa za maonesho kwenye tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne linalofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe jijini Dar es salaam linaloshirikisha watumishi wa wizara hiyo na taasisi zake.
Kikundi ncha ngoma kutoka Wizara ya Fedha wakicheza wakati wa mashindano ya sanaa za maonesho kwenye tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne linalofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe jijini Dar es salaam.
Kikundi cha shairi kutoka Wakala ya Huduma ya Manunuzi Serikalini (GPSA) wakiimba shairi wakati wa mashindano ya tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne linalofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akiwaaga watumishi mara baada ya kufungua tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne linalofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe jijini Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment