Mwenyekiti wa NATASA ,Given Massawe akipozi kwa picha na wadau wa NATASA, toka kushoto ni Henry Mzava,Evance,Letitia Smith ambae yeye anatoka Namibia, Henry,Hamza Riyani, Charles na Mercy.
M/kiti wa NATASA Given Massawe akikata keki ya ya kuzindua umoja huo pamoja kuazimisha miaka 53 ya Uhuru wa Tz huku katibu wake Halima Guga akishuhudia. Wakina dada wa Kitanzania wanaosoma kwenye mjii wa Nanchang ambao ni wanachama wa NATASA wakipozi kwa picha wakiwa na bendera zao za Tanzania siku ya uzinduzi huo. .Wakina dada wa Kitanzania wanaosoma kwenye mjii wa Nanchang ambao ni wanachama wa NATASA wakipozi kwa picha wakiwa na bendera zao za Tanzania siku ya uzinduzi huo. wadau wa NATASA wakiwa ndani ya ukumbi wa Hotel ya XIN DIAN TI wakibadilisha mawazo mawili matatu na kukumbushana story mbali mbali za nyumbani Tanzania. Mzee wa Shekeli Geofrey Njalangi na kitamba chake cheupe mkononi mbele kabisa akisataka rhumba siku ya uzinduzi huo wa NATASA pamoja na Charles kulia na Elvis kushoto kwake ndani ya ukumbi wa XIN DIAN TI HOTEL kwenye mjii wa Nanchang nchini CHINA. Mo van der Mhando,Nanchang, China.
j
U UWanafunzi wa Kitanzania wanaosoma kwenye mjii wa Nanchang nchini China wameanzisha umoja wao na Jumamosi iliyopita wameuzindua rasmi umoja huo wenye lengo la kuwasaidia kwa mambo mbali mbali
j
U UWanafunzi wa Kitanzania wanaosoma kwenye mjii wa Nanchang nchini China wameanzisha umoja wao na Jumamosi iliyopita wameuzindua rasmi umoja huo wenye lengo la kuwasaidia kwa mambo mbali mbali
wakiwa kwenye nchi ya kigeni.Jumla ya wanafunzi 54 wa Kitanzania wapo kwenye mjii huo wakiwa wanasoma kwenye vyuo mbali mbali na walikuwa hawana kitu chochote kinachowaweka karibu kama Watanzania na ndio maana wakaanzisha umoja huo.
Umoja huo unaojulikana kwa jina la Nanchang, Tanzanian Students Association (NATASA) ulizinduliwa rasmi na mwenyekiti wake Given Massawe ambae alisema kuanzishwa kwa umoja huo lilikuwa ni wazo la muda mrefu na hatimae hivi sasa ndoto imetimia.
Massawe alifafanua kuwa kwenye mingine ya nchini China ambako kuna wanafunzi wa Kitanzania nao wanajumuia zao ambazo zinawasaidia hivyo kwa wanafunzi wa Nanchang kuwa na umoja huo ni sehemu ya fungua milango kwao.
Massawe alifafanua kuwa kwenye mingine ya nchini China ambako kuna wanafunzi wa Kitanzania nao wanajumuia zao ambazo zinawasaidia hivyo kwa wanafunzi wa Nanchang kuwa na umoja huo ni sehemu ya fungua milango kwao.
Mwenyekiti huyo amesema hivi sasa wapo kwenye harakati za kutengeneza katiba yao ambayo ndio itakuwa dira ya uongozi wao na pia kuzinduliwa kwa chama hicho ni msaada tosha kwa wanafunzi hao wa Kitanzania kuanzia kwenye masomo hadi maisha ya kila siku.Uzinduzi wa umoja huo ulienda sambamba za sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania bara na hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa wanafunzi wa Nanchang kusherekea siku yao ya Uhuru wakiwa pamoja. Michuzi
0 comments:
Post a Comment