2015-01-09

Afunguka;Afande Sele Daz Baba havuti unga, anakunywa pombe kupita kiasi


Afande Sele: Daz Baba havuti unga, anakunywa pombe kupita kiasi
Afande Sele amedai kuwa Daz Baba havuti unga kama watu wengi wanavyodhani bali amekuwa akinywa pombe bila kuzingatia kula hali inayomfanya akonde. 



Akiongea na Bongo5, Afande amesema huu ni wakati wa wasanii na wadau wa muziki nchini kuonyesha juhudi za kumuokoa katika hali hiyo ili kunusuru maisha yake.


“Tatizo sisi wabongo tunapenda kusema vitu vya unafiki hasa hasa sisi wasanii,” amesema Afande. “Tunashindwa kusema vitu vya ukweli mwisho wake tunaathirika zaidi. Mbona wasanii wengine wa nje wakifilisika wanasema wamefilisika ili waweze kuishi maisha ya kawaida?” amehoji Afande.


“Tatizo watu wanajikweza wakati hawana kitu. Kusema kweli hali halisi ya Daz Baba ni mtu ambaye kama kachanganikiwa hivi. Daz Baba havuti unga. Wasanii acheni kuongea huu ndio wakati wa kumsaidia. Daz Baba akinywa pombe hata bia mbili tu anabadilika kabisa na tatizo lake Daz akinywa pombe hawezi kula, kwahiyo mara nyingi anakesha anakunywa pombe, hachagui pombe. Kusema kweli Daz Baba ni mtu ambaye kachakaa.


Mimi naapa Daz havuti unga ila ni mlevi kupita kiasi. Hana muda wa kulala. Ukikutana naye sehemu unamwomba msamaha wewe kwa sababu bila hivyo atakusumbua na haelewi anachoongea, kama vile chizi tu. Wapo wadau ambao wanajua Daz katoka wapi. Mimi mwenyewe binafsi nimeshahangaika na Daz na kwa namna ya pekee lakini watu wengine hawafikirii kama hili jambo ni la serious.”


“Toka naanza kubadilika mimi najaribu kumweka sawa. Kwasababu kama hali ngumu hata sisi hali ngumu tunahangaika tu. Watu wengi wanasubiria mtu amekufa halafu waanze kutoa magari na michango. Kwanini kama mnaweza kufanya juhudi hizo msifanye sasa hivi? Kwenye mazishi watu wanajifanya kukodi magari kwenda kuzika, mtu kama Daz kipindi hiki ndio cha kumsaidia. Wapo marafiki wa Daz, wasanii wadau wanaweza kumsaidia sasa hivi.”

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...