2015-01-21

Afunguka;Hizi ni Sentensi za Zitto Kabwe kuhusu yeye kurudi Chadema.


Mheshimiwa Zitto Kabwe ambaye ni mbunge wa Kigoma Kaskazini mwanzoni mwa mwaka 2014 alikua na mgogoro mkubwa na Chama chake cha Chadema. 


Magazeti yaliyotoka siku chache zilizopita yali ripoti taarifa ya Mbunge Zitto Kabwe kurudi tena Chadema,millardayo.com imepata exclusive interview na Zitto Kabwe na hizi ni sentensi zake. 

Swali lilikua ni yeye kuhusu kurudi Chadema>>’Hapana nadhani hizo ni tetesi kwa sababu sijatoa kauli yoyote kuhusiana na hilo na moja mimi bado mwanachama wa Chadema kwa sababu nina kesi mahakamani na kesi hiyo haijaamuliwa,bado inaendelea’ 

‘Sijawahi kutoka kwenye uanachama wa Chadema,mtu anaposema nataka kurudi Chadema hayuko sahihi,inafahamika nilikuwa na matatizo na chama hatujaweza kuyatatua,hakuna mazungumzo yoyote ambayo yamefanyika lakini kuna baadhi ya watu wameanza kuleta hayo mazungumzo’.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...