Rais
wa Benki ya Dunia Jim Yong Kim ametaadharisha amesema kuwa ni hatari
kwa kuwa dunia haijajiandaa kupambana na ugonjwa wa Ebola Afrika
Magharibi.
Akiongea mjini Washington,Kim,amesema ni muhimu kwa
Serikali, mashirika, Mashirika ya misaada na makampuni ya Bima kufanya
kazi pamoja kujiandaa kukabiliana na maradhi hayo siku za usoni.
Zaidi ya Watu 8,500 wamepoteza maisha hasa nchini sierra leone, Guinea na Liberia.
Kim
amesema Ebola imekuwa tishio ikizingatiwa idadi ya Watu waliopoteza
maisha na kuathiri uchumi hivyo amesema jitihada zifanyike kuutokomeza
kabisha ugonjwa wa Ebola na kuitaka dunia kujifunza kutokana na athari
za ugonjwa huu kwa kuwa dunia itakabiliwa na maradhi mengine miaka
ijayo.
bbc swahili
bbc swahili
0 comments:
Post a Comment