2015-01-28

Duuuuuuuuuuu; Mwanamke afikisha miaka 40 bila ndoa..hiki ndicho alichoamua!



Matukio ya wanawake kukata tamaa ya kuolewa kwa miaka ya sasa yameanza kuonekana ni ‘fashion’ huku wengi waaiona ni jambo la kawaida kuishi maisha ya peke yao. 


Yasmin Eleby mwenyeji wa Houston, Marekani ameamua kufunga ndoa ya peke yake baada ya kufikisha miaka 40 bila kuona dalili yoyote ya kuolewa.

Eleby aliamua kufanya siku yake hiyo kuwa ya tukio muhimu kama ambavyo alikua akiota siku moja atakuja kuolewa na kufurahia siku hiyo ambapo aliwaalika baadhi ya ndugu zake na marafiki na kuamua kufanya sherehe hiyo katika ukumbi wa makumbusho waHouston Museum. 

Taratibu zote za arusi zilifuatwa na wageni waliohudhuria wakiwemo ndugu wa karibu na walimsapoti na kufurahia sherehe hiyo.

Yasmin Eleby akiwa na wazazi wake siku ya harusi yake
Mwanamke huyo amepanga pia kwenda fungate ambapo atatembelea miji ya Laos, Cambodia, and Dubai.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...