Ommy Dimpoz akizungumza mbele ya wanafunzi wa Mbezi High School walipofika hapo na Idris kuwapa moyo na kutoa shukurani zao kwa kwa sapoti wanayoendelea kuwapa hususan katika fani yake ya muziki.
Mtangazaji wa Clouds FM, Millard Ayo, akiungana kwenye picha ya pamoja na walimu na wasanii hao.
MSANII wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz na mshindi wa Big Brother 2014, Idris Sultan, mapema leo walifanya tukio la kipekee baada ya kutinga katika shule ya Mbezi High School, waliosoma na kuwashitukiza walimu na wanafunzi kwa pamoja kabla hawajaingia kwenye vipindi vya masomo.
Wakizungumza katika ishu hiyo, Ommy Dmpoz na Idris walisema walikutana na kukaa pamoja na kujadiliana juu ya kwenda shuleni hapo kuwapa moyo na shukurani kwa ujumla walimu na wanafunzi wa shule hiyo ambayo walisoma.
“Tumekaa na tukapanga hili wazo ili tuweze kuwashukuru kwa yote mnayotutendea, hususani kufuatia ushindi wangu wa Big Brother, ambao naamini kabisa kwa vyovyote mchango wenu ulikuwa mkubwa kwangu.
Mwenzangu Ommy Dimpoz alitangulia kumaliza shule kabla yangu, ila mmekuwa mkimsapoti kwa kila anachokifanya kwenye muziki wake,” alisema Idris.
GPL
GPL
0 comments:
Post a Comment