2015-01-26

Ni Aibuuuuuu!!!!!!!!! Diwani wa CCM Afumaniwa Gesti na Mwanafunzi Wakibanjuka, Wananchi walimnusura Wampe Kichapo


 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida diwani wa kata ya Nyugwa katika halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale mkoani mkoani Donald Kabosolo (CCM) amenusurika kupigwa na wananchi wenye hasira kali mara baada ya kukutwa akifanya mapenzi na mwanafunzi Nyugwa sekondari.

Tukio hilo la aina yake lililoshangaza na kusikitisha wananchi wa mjini hapo na viunga vyake lilitokea jana majira ya jioni baada ya diwani huyo kumchukua mwanafunzi huyo (Jina Tunalihifadhi) wa kidato cha tatu kwa ajili ya kufanya nae mapenzi kwenye gesti ya diwani huyo iliyopo mjini Kharumwa.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa diwani huyo alikuwa kwenye nyumba yake ya kulala wageni hapo majira ya jioni lakini baada ya muda walimuona mwanafunzi akifika hapo na kuingia ndani kwa muda mrefu ndipo walipoweka mtego wa kumnasa kwa vile wananchi wanadai kuwa alikuwa anafanya nae mapenzi kwa muda mrefu. 


"Ninashangaa kumuona diwani huyo ambaye ni kioo cha jamii anafanya mapenzi na mwanafunzi , kama anataka mwanafunzi angeenda vyuoni ambako kule wanasoma wameolewa na si hapa kwetu tena kwenye kata yake, huyu anatakiwa achukuliwe hatua za kisheria’’alisema mwananchi huyo.

Hata hivyo diwani huyo baada ya kukamatwa na wananchi huku wakitaka kumshushia kipigo, baadhi ya wasamaria wema waliwataarifu jeshi la polisi ambapo walifika na kumpeleka kituoni kwa usalama wake kabla ya kuwekewa dhamana.

Alipotafutwa diwani huyo kwa njia ya simu yake ya kiganjani alisema kuwa anasikitishwa na mpango ambao huo umesukwa kutokana na mambo mengi aliyoyaibua katika shule hiyo yaliyokuwa yakifanywa na baadhi ya viongozi wa shule.

"Mwandishi mimi nashangaa kwamba nimekamatwa na mwanafunzi wa kidato cha tatu tena wa shule yangu sijakamatwa hata kidogo lakini kuna mambo mengi yalikuwa yanafanywa na viongozi wa shule hiyo kwa kufisadi mambo katika shule hiyo ndio maana wameamua kunisigizia’’ alisema diwani. 


Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye ni mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale Ibrahimu Marwa, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa atahakikisha diwani huyo anachukuliwa hatua mara moja na wale watakao onekana kumtetea na wao watachukuliwa hatua.

“Ni kweli diwani amefanya, kitendo hicho si cha kiungwana kabisa kwani amejidhalilisha yeye mwenye, familia yake na chama chake nitahakikisha anachukuliwa hatua mara moja,”alisema Marwa

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...