HOFU! Waigizaji wa tasnia ya filamu Tanzania, ambao walikuwa wameanza kusahausahau misiba mfululizo iliyowatokea miaka michache iliyopita, juzikati walijikuta wakitoneshwa kidonda, baada ya kutokea kifo cha muigizaji Tino Madhahabu, kilichotokea Tunduma mkoani Mbeya, kufuatia kuugua kwa muda mrefu.
Muigizaji Tino Madhahabu enzi za uhai wake.
Muigizaji Tino Madhahabu enzi za uhai wake.
Msanii huyo aliyetamba katika uigizaji akiwa na Dude katika kipindi maarufu cha Bongo Dar es Salaam, kwa muda wa miaka saba na baadaye kuingia kwenye filamu alikuwa akiugua ugonjwa wa moyo, kiasi cha kumfanya arejee nyumbani kwao kwa ajili ya matibabu, ambayo hata hivyo, yameshindwa kunusuru uhai wake.
Msanii 'Dude' aliyewahi kuigiza na Tino katiaka kipindi maarafu cha Bongo Dar es Salaam.
Kifo hicho kimeibua hofu upya kwa wasanii wa Bongo Muvi, hasa ikikumbukwa kuwa mchunguji mmoja (jina tunalihifadhi) aliwahi kutabiri kuwa, wimbi hilo la vifo litaendelea tena mwaka huu kwa wasanii na watu wengine maarufu, wakiwemo wanasiasa hivyo kuwataka kumrudia Mungu.
Msanii wa filamu Bongo Jini kabula.
Wasanii kadhaa waliozungumza na Ijumaa baada ya taarifa za msiba huo walionesha hofu ya kifo waliyonayo lakini wengi wakasema Kifo cha Tino ni mipango ya Mungu hivyo kila mmoja ajiandae tu.
Msanii aliyewahi kufanya kazi kwa karibu na Tino, Kulwa Kikumba ‘Dude’ alisema: “ Dah! Ni kweli jamaa katutoka, kikubwa tumuombee na hilo la hofu ni vyema kila mmoja akawa nayo ili aweze kujiandaa kwa safari.”
Msanii wa filamu Bongo, Devota Mbaga.
Katika kuonesha kuweweseka, msanii mwingine wa filamu, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ alisema: “Mimi sitakufa kwa kuwa niko karibu na Mungu, watakaokufa ni wale walio mbali na Mungu.”
Msanii mwingine, Isabela alisema kifo cha Tino kimemshtua mno na kusema ni mapenzi ya Mungu, lakini akaponda utabiri wa mchungaji akisema hajawahi kuamini mambo hayo, kauli ambayo pia ilitolewa na Rose Ndauka.
Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, kulikuwa hakuna taarifa rasmi zilizotolewa juu ya mazishi ya msanii huyo.Mungu Ilaze roho ya Marehemu mahali pema peponi.
Msanii huyo aliwahi kuhojiwa na Global TV Online akizungumzia ugonjwa wake pamoja na kuomba msaada hivyo ukitaka kuyasikia, fungua mtandao wa www.globaltvtz.com
GPL.
0 comments:
Post a Comment