Waziri wa maji Jumanne Maghembe (wa kwanza kulia) akizungumza na wakandarasi wanaojenga bomba la maji la Mlandizi Kimara Januari 20, 2015 mkoani Pwani wakati alipotembelea tembelea miradi ya maji inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na maji Taka (DAWASA), kwa lengo la kupata tathimini ya mradi huo ulipofikia sasa.(Habari Picha na Philemon Solomon).
WAZIRI wa maji Jumanne Maghembe ametoa siku 90, kwa mkandarasi Megha Engineering Infrastructure Limited anaesambaza bomba la maji mradi wa Mlandizi Kimara kufanikisha mradi huo na kupeleka ripoti ya mradi,mamlaka ya maji safi na maji taka (Dawasco), kwa lengo la kupata tathimini ya mradi.
Alitoa agizo hilo Januari 20, 2015 mkoani Pwani wakati akikagua miradi minne ya Dawasco,yakusambaza maji Ruvu juu na Ruvu chini kufikisha Jijini Dar es Salaam.
Alisema,mpaka sasa mkandarasi alitakiwa aweamelaza kilomita 20,lakini cha kushangaza mkandarasi huyo amelaza kilomita 12, tu.
Waziri wa maji Jumanne Mghembe (wa pili kulia) akiwa ameongozana na Meneja mradi Pintu Dutta (wa tatu kulia) wakati akikagua maendeleo ya mradi wa kituo cha kusafisha maji cha Ruvu juu.
Maghembe alisema utendaji kazi wa mkandarasi huyo ni mbovu na nimewaagiza wabadilike na nitakuja kuwatembelea baada ya siku 90, na kama hakutakuwa na maendeleo itabidi tuwafukuze.
“tumempatia mkandarasi huyu kiasi cha shilingi bilioni 96 za kitanzania fedha hizi watanzania watazilipa hivyo ni vema mkandarasi huyu afanye kazi iliyomleta,”alisema Maghembe
Kwa upande wa mradi wa Ruvu juu wa kusafisha maji Waziri Maghembe aliridhika na utendaji kazi wa mkandarasi anayejenga mradi huo na kumtaka amalizie kufunga pampu mpya ili mgao wa maji upungue Dar es Salaam.
Aidha alimwagiza Mkurugenzi Mkuu wa DAWASA Arcado Mutalemwa kuhakikisha pampu zilizokwama bandarini zinafika leo na kufungwa siku ya Alhamisi.
Waziri wa Maji Jumanne Maghembe (wa pili kulia) akioneshwa mchoro wa mradi wa bomba la maji Mlandizi Kimara linalopitia Makongo juu na Mhandisi wa Mradi huo, Bw Severin Mkendala jinsi mabomba mradi wa Mlandizi Kimara yalipopita .
Wafanyakazi wa kampuni ya WABAG Constraction wakiendela na ujenzi wa wa kituo cha kusafisha maji cha Ruvu juu .
Gari aina ya Caterpillar la kampuni ya Megha Engineering Infrastructure Limited, likiwa linasafisha eneo ambalo linatakiwa kulazwa mabomba ya yanayotoka Mlandizi Kimara kwenda Ruvu juu.
Kushoto ni Meneja Mradi kutoka Kampuni ya Megha Engineering Infrastructure Limited Mural Mohan, akimweleza maendeleo ya mradi huo Waziri wa Maji Jumanne Maghembe, aliyekuwa katika ziara ya kutembelea miradi inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka.
Waziri wa Maji Jumanne Maghembe akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukamilisha ziara hiyo.
0 comments:
Post a Comment