Askari wa kituo kikuu cha Shinyanga aliyefahamika kwa jina moja la Alex,amewekwa korokoroni akituhumiwa kumbaka mwanafunzi wa kidato cha kwanza mkazi wa kata ya Ngokolo na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za siri.
Kamanda wa Polisi Shinyanga Justus Kamugisha alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili kubaini ukweli kamili.
“Tunaendelea kufanya uchunguzi lakini sina haja ya kutaja jina lake kwa sasa hadi tutakapokamilisha upelelezi wetu na kujiridhisha”alisema.
Mama mdogo wa mwanafunzi huyo akisimulia mkasa huo alisema mwanaye alitoka usiku kwenda kujisaidia na ndipo alipokutana na askari huyo ambaye aimvutia chumbani kwake kisha kutekeleza unyama huo.
0 comments:
Post a Comment