2015-01-21

Mambo Hayo;Hii ya Romario wa Brazil na mpenzi wake mpya nayo imo leo…. miaka 19?


Mshambuliaji nyota wa zamani wa Brazil Romario ametoa kali ya mwaka baada ya kuanza uhusiano nab inti mdogo mwenye umri kama wa kumzaa mwenyewe. 


Romario anadhaniwa kuwa alianza uhusiano na mrembo mwenye umri wa miaka 19 Dixxie Pratt ambaye ni raia wa Marekani siku hache baada ya kuachana na mkewe mwaka 2014 .

Romario mwenye umri wa miaka 48 akiwa na mpenzi wake mpya mwenye umri wa miaka 19. 

Romario mwenye umri wa miaka 48 amemzidi Dixie kwa miaka 30 na binti huyo wala hakuwa amezaliwa wakati Romario akiiongoza Brazil kutwaa ubingwa wa dunia mwaka 1994 ambapo alikuwa moja kati ya wafungaji bora . 

Romario atakumbukwa sana kwa mabao yake akiwa na timu ya taifa ya Brazil pamoja na klabu kadhaa ikiwemo Barcelona ambayo aliichezea baada ya kutwaa kombe la dunia mwaka 1994 .

Romario na mpenzi wake aitwaye Dixie wakiwa mazoezini kwenye ufukwe wa bahari huko Brazil. 

Hivi karibuni kurasa mbalimbali binafsi za Mitandao ya kijamii za Romario zimekuwa zikirusha picha mbalimbali zikiwaonyesha Romario na Dixie wakiwa kwenye furaha ndani ya uhusiano wao .

Hapa wakiwa ‘viwanja’ kwenye ‘bata’.


Wakati Romario akiisaidia Brazil kutwaa ubingwa mwaka 1994 , mpenzi wake wa sasa Dixie alikuwa hajazaliwa.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...