Waziri wa usalama nchini Kenya, Joseph Nkaissery amewaomba radhi wanafunzi wa shule ya msingi ya Lang’ata baada ya kupigwa mabomu ya machozi jana walipoandamana kupinga kunyang’anywa kipande cha ardhi ambacho kilikuwa uwanja wao wa kuchezea.“Jana hata hawataki tusherehekee, tukicheza wanatupiga na rungu wanatuletea madogi”–Mwanafunzi.
Waziri wa usalama Kenya, Joseph Nkaissery.
Rais Uhuru Kenyatta amelaani tukio hilo na kumtaka Waziri wa Ardhi, Charity Ngilu na Mwenyekiti wa Tume ya Ardhi, Mohammed Swazuri kuwajibika na kueleza kwanini walizembea, huku Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo pia kalaumiwa kwa kusindwa kuzuia watoto hao kujihusisha na vurugu.
Bado haijafahamika ni nani aliyehusika na ujenzi huo.
Nimekuwekea hapa taarifa hiyo niliyokurekodia kutoka kituo cha K24 pamojja na video ya story hiyo.
0 comments:
Post a Comment