Victor Valdes ametambulishwa rasmi kama mchezaji wa Manchester United ambapo kipa huyo wa zamani wa Barcelona amesema ana furaha kubwa kujinga na Mashetani Wekundu, timu yenye mvuto wa aina yake.Valdes mwenye umri wa miaka 32,
amesaini mkataba wa miezi 18 huku kukiwa na kipengele kinachoweza kurefusha mkataba huo kwa mwaka mmoja zaidi.
“Kwa mara ya kwanza nilipokuja hapa kwenye uwanja wa mazoezi - Aon Training Complex, nikaona maandishi makubwa mekundu ya Manchester United. “Kwangu mimi ilikuwa kama njozi. Nimecheza Barcelona kwa miaka mingi, ni klabu kubwa na niliipenda kwa maisha yangu

yote.“Nadhani hali hiyo imejirudia tena hapa. United ni klabu kubwa duniani na ina mashabiki wengi kila kona.“Nilifanya kazi na Louis van Gaal FC Barcelona. Kupata nafasi ya kufanya naye kazi tena hapa Manchester United, ni njozi iliyotimia,” alisema Victor Valdes.
0 comments:
Post a Comment