MGOMBEA wa Chama cha Patriotic Front, Edga Lungu ameshinda uchaguzi wa urais nchini Zambia.
Tume ya uchaguzi nchini humo imesema kuwa Lungu amepata asilimia 48 ya kura zilizopigwa.
Alikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mgombea wa upinzani Hakainde Hichilema.
Wagombea wote wawili walikuwa wameahidi kuboresha mifumo ya elimu na kubuni nafasi za ajira.
Uchaguzi huo uliandaliwa kufuatia kifo cha rais Michael Sata aliyefariki dunia mwezi Oktoba mwaka jana.
GPL
0 comments:
Post a Comment