Nimewezesha kupatikana kwa wawekezaji mbalimbali waliokuja kuwekeza katika wilaya hii ya Hanang’ na pia nimewezesha kupatikana kwa mkopo nafuu wa matrekta mapya 70
1. Robert Sulle, mchimbaji mdogo wa madini ya chumvi kwenye Kijiji cha Gendabi.
Uwezeshaji wa mgodi wa chumvi umefikia hatua gani?
Jibu: Katika mradi wa chumvi wa Kijiji cha Gendabi tutahakikisha tunawashirikisha wachimbaji wadogo tuone namna ya kuendeleza eneo hilo kwa kuhakikisha wafanyabiashara wanaokuja kununua chumvi hiyo wananunua kwa bei ambayo itamnufaisha mchimbaji mdogo wa eneo hilo na suala la kuongeza thamani chumvi hiyo ili kuwepo na madini joto bado wataalam wanalishuhulikia na endapo kuna wawekezaji watataka kuwekeza tutawashirikisha kwanza wachimbaji wadogo ili waridhie uwekezaji huo.

2.John Clet mkulima na mkazi wa Kitongoji cha Jorodomu, Kata ya Ganana.
Mikopo ya matrekta uliyotoa kwenye baadhi ya vijiji vya wilaya hii, imewanufaishaje wakulima?
Jibu: Mikopo ya matrekta imechangia kwa kiasi kikubwa wakulima wa eneo hili wapige hatua kwenye maendeleo kwani imewawezesha walime ekari nyingi zaidi tofauti na awali na matrekta hayo mapya zaidi ya 70 yamefanikisha wilaya ya Hanang’ kuwa na chakula kingi kila wakati wa msimu, kwani mazao yamevunwa kwa wingi tofauti na awali kabla matrekta hayo hayajapatikana.
3. Amina Ramadhan mkazi wa kata ya Endasak.
Soko la kimataifa kwenye kata ya Endasak limefikia hatua gani?
Jibu:Hivi sasa mradi huo umefikia kwenye hatua nzuri kwani fedha za awali za uanzishaji wa soko hilo ndiyo zinasubiriwa kutolewa na eneo la kujenga soko hilo limeshapatikana kwenye mnada wa zamani wa kijiji cha Endagaw kata ya Endasak ambapo soko hilo litawanufaisha wakulima wengi na mwaka huu wa fedha wa 2014/2015 ujenzi utaanza.
7. Martin Gapchojiga, mkulima wa Kata ya Gidahababieg
Wewe kama mbunge wa Jimbo la Hanang’ unadhani wananchi wa wilaya hii watakukumbuka kwa jambo lipi? kwani wilaya hii tulishapata viongozi wengi wakubwa, akiwemo Waziri Mkuu lakini hakuacha jambo la kukumbukwa.
Jibu: Wakazi wa Hanang’ watanikumbuka kwa mambo mengi sana ya maendeleo kwani wakati naingia kwenye ubunge wangu mwaka 2005 kulikuwa na changamoto nyingi ambapo kwa kushirikiana na wananchi tumeweza kuzitatua, kulikuwa na visima nane virefu mwaka 2005 sasa kuna visima 42, kulikuwa na visima viwili vifupi sasa vipo tisa, mwaka 2005 kulikuwa na kata nne zenye maji ya bomba leo kata 17 zinapata uhakika wa maji ya bomba na kata nyingine zinapata maji ya visima virefu na vifupi pamoja na mabwawa yaliyochimbwa kwa ajili ya mifugo, kata nne zilikuwa na miundombinu ya barabara na sasa kata zote 25 zina barabara zinazopitika kwa kipindi chote cha mwaka isipokuwa kata moja ya Lalaji, kulikuwa na shule sita za sekondari mwaka 2005 na leo kuna shule 34 ikiwemo moja ya binafsi, kulikuwa na shule 72 za msingi leo zipo 115, kituo cha afya kilikuwa kimoja Katesh sasa vipo vituo vya afya vinne ikiwemo kimoja cha Mission Balang’dalalu, zahanati zilikuwa
11 leo zipo 24 pia niwe wawezesha mkopo wa matrekta mapya 70, uwezeshaji wa mazao ya kilimo umeongezeka mno kila msimu wa kilimo unapowadia kutokana na kulima kitaalamu na pia wakulima wanatumia mbegu bora za kisasa.
0 comments:
Post a Comment