Kongozi wa kundi la Boko Haram Abubakar Shekau amedai kuwa wapiganaji wa kundi hilo ndio waliofanya shambulio katika mji wa Baga kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Katika ujumbe wa video aliouwasilisha kwenye mtandao, Shekau pia amezitishia Chad na Cameroon.
Shekau ameutoa ujumbe huo wakati ambapo wajumbe wa Nigeria na jirani zao walikutana katika mji mkuu wa Niger, Niamey kujadili njia za kuuratibisha mkakati wa pamoja wa kuwakabili magaidi wa Boko Haram.
Habari zaidi zinasema, jana usiku yalitokea mapambano makali baina ya wapiganaji wa Boko Haram na wanajeshi wa Cameroon kwenye kijiji cha mpakani, Bonderi kilichopo kaskazini mwa Cameroon.
0 comments:
Post a Comment