2015-02-05

VIDEO: RAIS MUGABE ADONDOKA UWANJA WA NDEGE..........cheki watu wakimshangaa,,,,,,,,,,bofya hapa kuona


Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, akidondoka kwenye uwanja wa ndege Harare.

RAIS wa Zimbabwe, Robert Mugabe jana, Februari 4, mwaka huu alidondoka akiwa uwanja wa ndege muda mfupi akitokea nchini Ethiopia. 



Rais Mugabe alikuwa akiwahutubia wafuasi wake katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Harare ila wakati akishuka jukwaani aliteleza na kuanguka.

Mugabe alinyanyuliwa haraka na wasaidizi wake kisha kupelekwa kwenye gari na kuondoka eneo hilo, mmoja wa mashuhuda alieleza.

"Alikuwa akiwahutubia wafuasi wake waliofika kumpokea, akateleza wakati akishuka ngazi na kudondoka chini" shuhuda huyo alisema 


Baadhi ya wanahabari waliochukua tukio hilo walidai kulazaimishwa na maofisa usalama kufuta picha hizo kutoka kwenye kamera zao.

Mugabe alikuwa akioka nchini Ethiopia kwenye mkutano wa viongozi wa nchi za Umoja wa Afrika (AU) ambapo alichaguliwa kuwa mwenyekti wa mkutano huo. 
GPL

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...