2015-02-18

Chenge: Mimi ni nyoka, Asema ni yule mwenye makengeza, Asisitiza kuwa ni mtafuta fedha.......fuatilia kisa hapa

 
 Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge, ‘amefunguka’ kuhusu kashfa inayomkabili ya kupata mgawo wa Sh. bilioni 1.6 kutoka kwenye fedha zilizochotwa kifisadi katika akaunti ya Tegeta Escrow, iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), akisema hastahili kuitwa mwizi, bali anapaswa kuitwa ‘nyoka wa makengeza’.

Amesema anapaswa kuitwa ‘nyoka wa makengeza’ kwa kuwa yeye ni mjanja wa kutafuta fedha kwa ajili ya wananchi wa jimbo lake, ambao wanapaswa kupuuza madai ya wizi yanayoelekezwa kwake, badala yake wamwamini zaidi.


Chenge, ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) mstaafu, alisema hayo wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Mahaha kata ya Bunamala, Wilaya Bariadi mkoani Simiyu juzi.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...