2015-02-24

Daaaaaaaaaaaa Aliyewalawiti Watoto Kenya kuhukumiwa



Raia wa Uingereza aliyewadhalilisha kingono watoto wa kiume katika mji mdogo wa Gilgil nchini Kenya anatarajiwa kuhukumiwa leo

Raia wa Uingereza Simon Harris, aliyedhalalisha kingono watoto waliokuwa wakirandaranda mitaani katika mji mdogo wa Gilgil nchini Kenya atahukumiwa leo nchini Uingereza.

Hii ni baada ya mahakama ya Birmingham kumpata na hatia ya kudhalalisha kingono watoto wa kiume na kupatikana na picha za utupu za watoto.

Harris mwenye umri wa miaka 55 alikuwa akiendesha mradi wa kutoa misaada kwa jamii na alikuawa mtu aliyeheshimika.

Hatahivyo alitumia nafasi hiyo kuwashawishi watoto.a

Kwa takriban miaka 20 alikuwa akitumia gari lake kuzunguka katika mitaa ya Gilgil,

nia yake ikiwa kunyemelea watoto wa kiume waliokuwa wakirandaranda mitaani, kwa kisingizio kuwa alijali na kushugulikia maslahi yao.

Polisi wanasema waathirika 40 walijitokeza kutoa ushahidi.

Hatahivyo ili kufanikisha utaratibu wa mahakama ushahidi wa 11 kati yao ndiyo uliotumika.

Waathirika walitoa ushahidi katika mahakama hiyo ya Uingereza kupitia mtambo wa video uliowekwa nchini Kenya.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...