Siku chache zilizopita UNAIDS ilimpa heshima mwanamke huyu aliyejibadili jinsia kuwa Balozi wake.
Alizaliwa Luanda kama Teca Miguel Garcia, akiwa muimbaji na mchezaji, Titica alibadili maumbile yake miaka minne iliyopita mara
baaada kufanya upasuaji wa maziwa nchini Brazil.
Sasa, akiwa na miaka 26, Titica amekuwa kioo cha Angola kwa aina ya muziki anaoufanya
wenye mchanganyiko wa miondoko ya rap na
techno unaojulikana kama “kuduro”.
Akiongea na BBC mwaka jana, akiwa kwenye kwenye utengenezwaji wa video ya wimbo wake unaotamba sasa uitwao Olha o Boneco, wimbo
ambao amemshirikisha muimbaji mashuhuri wa muziki aina ya kizomba aitwaye Ary, Titica alisema amefanikiwa kukabiliana na vikwazo vyake.
“Shukrani kwa Mungu, nina furaha sana, imechukua muda kufika hapa na imehusisha mambo mengi ya kujitolea ila asante Mungu,
kila kitu kinakwenda sawa kwangu.
0 comments:
Post a Comment