2015-02-13

Filamu inayoonyesha hadi mambo ya chumbani, yapigwa MARUFUKU

Fifty shades of grey


Bodi ya Uainishaji wa filamu nchini Kenya imepiga marufuku usambazaji na uuzaji wa filamu Fifty Shades of kwa madai kuwa inaonyesha mwanamke kama mtumwa wa ngono, ina picha za uchi za mwanamke na kuonyesha mambo ya kimapenzi kwa uwazi.

Bodi hiyo ya kudhibiti filamu imewaonya yeyote atakayepatikana akisambaza filamu hiyo atakabiliwa na shtaka la kueneza sinema zenye kuwaonesha watu watu wakiwa tupu na wengine wakistarehe kwa mifumo tofauti.

Mwenye kiti wa Bodi hiyo Askofu Jackson Kosgey alisema kwamba

"Licha ya kuwa filamu ambayo inaleta taswira ya ngono, kwa picha na sauti, ni moja ya filamu nyingi zinazoendeleza kampeni ya watu kukubali kwamba ngono ni jambo la kawaida tu kwa jamii ilhali huo ni ukiukaji wa haki za kibinadamu kulingana na sheria za Kenya. ‘’

Licha ya onyo hilo mashabiki wa filamu hiyo iliyotokana na riwaya kwa jina kama hilo walisema kuwa wataendelea kuitazama aghalabu kisirisiri majumbani mwao. bbc swahili

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...