2015-04-10

Dimpozi: Nje nafuata fedha, mzimu wangu upo bongo


MSANII wa bongo fleva, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, ameweka wazi kwamba huwa anakwenda katika maonyesho nchi za nje kwa sababu ya fedha, si mapenzi na nchi hizo.

Amesema hata akifika katika nchi hizo huwa anatamani kurudi mapema Tanzania, jambo ambalo huwa linamshangaza kila wakati.


Msanii huyo aliliambia MTANZANIA kwamba kinachompa kiburi cha kuendelea kufurahia nchi hii ni kutokana na amani na uhuru anaoupata, tofauti na anapokuwa katika maonyesho yake nchi za nje.

“Nimekuwa nikiandamwa na mzimu wa kukumbuka nyumbani, hivyo ndivyo ninavyoweza kusema, asikwambie mtu, nyumbani ni nyumbani, hata kama nje kuna raha kiasi gani,” alisema Ommy Dimpoz.

Ommy Dimpoz ameendelea kufanya vizuri kupitia wimbo na video yake ya ‘Wanjera’, ambao video yake imeshirikisha watu mbalimbali maarufu, akiwemo mwigizaji Wema Sepetu na mshindi wa Big Brother Africa (BBA) mwaka jana, Idriss Sultan.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...