Wakati akiendelea kutumikia kifungo akiwa jela huko Macau, Hong Kong nchini China, modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’ amenena mazito juu ya Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mwandani wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Juma Khalid ‘Jux’, Vanessa Mdee, Aunt Ezekiel na Moze Iyobo.
Modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’.
BARUA KUTOKA CHINA
Jack aliyekamatwa nchini humo kwa msala wa madawa ya kulevya ‘unga’ mwaka 2013 kisha kufungwa miaka sita kwenye Gereza la Macau, hivi karibuni alilitumia gazeti hili barua nzito akionesha kushtushwa na vitu fulani vya mastaa hao.
MIMBA YA AUNT
Moja kati ya mambo yaliyomshtua Jack ni mimba ya mwigizaji Aunt Ezekiel ambaye ni mke wa mtu, Sunday Demonte anayodaiwa kupachikwa na mcheza shoo wa Diamond, Moze Iyobo.
Hata hivyo, katika skendo hiyo, Jack aliwataka watu wamuache Aunt apumzike kwani mapenzi hayachagui hasa kama ana furaha.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Wema Sepetu.
“Nimeshtushwa na udaku special Lol! Sasa Aunt ameamua kutulia na Iyobo…acha apumzike mapenzi hayachagui as long as ndiyo furaha yake, that’s okey,” aliandika Jack.
DIAMOND, ZARI
Mbali na mimba hiyo ya Aunt inayoelekea kuzaa matunda muda si mrefu, modo huyo alionesha kushtushwa na penzi la staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz na Zari akishangaa ilikuwaje hadi jamaa huyo akaachana na Wema Sepetu kisha kutua kwa mrembo huyo mwenye maskani yake nchini Afrika Kusini na Uganda.
“Heh! Kwani Diamond aliachana na Wema tena?” Alihoji Jack na kuongeza:
“Sasa Zari si anakaa South Africa ‘Sauzi’? Wanaonana vipi na Platnumz? Mh! Wala hawatadumu maana mapenzi ya mbalimbali. Labda kama Nasibu (Diamond Platnumz) atahamia South.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mwandani wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ wakiwa kwenye pozi.
KAJALA Vs WEMA
Pia video queen huyo wa Ngoma za Nataka Kulewa (ya Diamond), She Got A Gwan (ya Marehemu Ngwea) na Kamugisha (ya Linex) aliulizia lile bifu zito la Wema na Kajala Masanja kama lilikwisha kwani mastaa wa Bongo Movies walishazoeleka kugombana na kupatana.
Bifu hilo ni lile la Wema kumtuhumu Kajala kumchukulia bwana’ke (CK) huku akisahahu kwamba alimlipia Sh. Milioni 13 ili asiende jela miaka mitano baada ya kukutwa na hatia ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.“Ya Kay (Kajala) na Wema naona mwishowe watarudisha urafiki tu. Ya Bongo Movies nimeshayazoea huwa wako hivyo kila muda, kawaida yao.”
JUX, VANESSA
Jack alipofika kwenye ishu ya kusalitiwa na staa wa Bongo Fleva, Jux akidaiwa kuwa kwenye malovee na sexy lady wa muziki wa Kizazi Kipya, Vanessa ‘Vee Money’, aliandika ishu hiyo kwa hisia zaidi huku akijilaumu mwenyewe kwa kosa alilofanya.
Juma Khalid ‘Jux’, akiwa na mpenzi wake Vanessa Mdee.
“Ya Jux na Vanessa nimeamua tu kuyaacha coz nipo jela siwezi kumzuia kufanya lolote then ni makosa yangu yaliyofanya hayo yote kutokea.“Sijui hata kama itakuja kutokea tena kuwa wote tena mimi na yeye, that chapter closed already, nahesabia muda mfupi tu now nitatoka lakini sina chochote cha kufanya nionane naye,” alimalizia kuandika Jack. Jack Patrick alihukumiwa kifungo hicho mwaka jana lakini taarifa zilieleza kuwa endapo ataonesha nidhamu gerezani ataachiwa mapenzi hivyo hatakaa jela miaka yote sita
0 comments:
Post a Comment