Lady Jaydee ametoa nafasi kwa mashabiki na followers wake wa Instagram kumuuliza maswali na kuahidi kuyajibu. Miongoni mwa maswali mengi aliyoulizwa ni pamaoja na kwanini hafanyi collabo na wasanii wa kike, na kuhusu Ugomvi / Tofauti na watu (wasanii) /Radio na mpango wa kupatana nao.
“Duuuh maswali yako mengi sana karibia 300 Ila ki ukweli yote yanafanana So, what i will do I will pick top 10 ya maswali yaliojirudia, halafu nitalijibu moja baada ya jingine. Watu wooote nikiwakusanya, maswali yenu hayazidi 10, Leo mtaelewa kwanini sijibu comments. Sababu nikifanya hivyo itabidi niache kazi zote, Kaeni tayari kwa majibu, moja baada ya jingine” aliandika Jaydee kabla hajaanza kuyajibu.
Haya ni baadhi ya maswali na majibu.
Swali: Kwanini sifanyi collabo na wasanii wa kike?
Jibu :
“Nimewahi kufanya na wasanii mbali mbali wa kike ila sijui kwanini hamjaziskia.
1.Mwasiti amewahi kunishirikiisha
2. Nimewahi kumuandikia na kushiriki kuimba kwenye wimbo wa movements za Albino na Kaysha
3. Nimewahi kumwandikia na kushiriki kuimba nae Nakaaya Sumari
4. Nimewahi kumwandikia wimbo Patricia Hillary
5. Nimewahi kumshirikisha RAY C kwenye wimbo wangu toka Album ya Machozi unaitwa, Nimekubali na wapo wasichana mbali mbali waliopita Machozi Band na kujifunza kuimba leo mnawafahamu.
Kumbukeni tu kuwa kutoka kwa mtu itategemea na nyimbo zake kuwa promoted redioni na mimi sio mwenye hizo redio.
Msaada pekee ni kushiriki kila ntakapotakiwa kufanya hivyo”
Swali: Ugomvi / Tofauti na watu Artists /Radio Na mpango wa kupatana nao
JIBU :
“Nitapatana na mtu atakae kubali kuwa alikosa, km naamini yeye ndio alinikosea itabidi aniombe msamaha. Kama mimi ndio nilikosa nitaomba pia msamaha,Otherwise hakuna miujiza.Siwezi kumuomba mtu msamaha endapo naamini kabisa sijakosa .
Niliowahi kuwakosea nilishawaomba msamaha wooote.Hakuna binadamu asie kosea Ila siwezi ku surrender kiuongo au kwa uoga wa maisha.
Naamini hata nikiuza nyanya bado wapo watu wanaohitaji nyanya, na watanunua. Je! Hili jibu limejitosheleza?.Naamini hata nyinyi mmewahi kutofautiana na watu wenu wa karibu.
Kukubali kosa ndio mpango”
Swali: Siasa
Mchango katika jamii
JIBU:
“Sio mpenzi na sitegemei kujihusisha na siasa, wala chama chochote. Kila binadamu ana mchango katika jamii kwa njia moja au nyingine, Direct au indirect.
Ukitambua moja lolote nililowahi kulifanya likakupa furaha ndio mchango wangu, samahani kwa yaliokuudhi.
Swali la 4 mpk la 10 ntamalizia kesho, yasipoisha hata kesho kutwa.Najua kuna maswali mazito mnayosubiria majibu, yale ya kidaku zaidi. …Na mimi kwa kuwarusha roho nayaweka mwiiiishooo.Yatajibiwa tu, msitie shaka. …”
GPL
0 comments:
Post a Comment