2015-02-14

MAKAVU LIVE: Baba kanumba amchana live Mama Kanumba, asema ana laana. !!!!Je ya kanumba? fuatilia!!!




BABA wa marehemu Steven Kanumba, Charles Kanumba amemchana mzazi mwenzake, Flora Mtegoa kuwa anateswa na laana na ndiyo maana hafanikiwi. 

Baba wa marehemu Steven Kanumba, Charles Kanumba. 

Mzee huyo alisema mama Kanumba ameshindwa kufanikiwa katika mambo mengi likiwemo suala la kuendeleza ofisi ya marehemu kutokana na kushindwa kumshirikisha yeye kama baba na ndiyo maana amepata laana. 

“Tatizo ni papara ya mwezangu ya kutaka mali ndiyo mambo yanayotokea na kamwe hataweza kufanikiwa kwa sababu baraka za mtoto zinatoka kwa mama na baba na hiyo laana itazidi kummaliza sababu hakunishirikisha,” alisema. 

Mama Kanumba Flora Mtegoa. 

Alipotafutwa mama Kanumba kuhusiana tuhuma hizo, alisema:
“Huyo mzee yeye ndiyo ana laana, nimeshamzoea, hana jipya amekalia majungu. Mimi sina laana, nakaa kwenye nyumba ya maana na si kama yeye anayeishi kwenye nyumba ya udongo.” GPL


Kingwendu msanii maarufu wa sanaa ya vichekesho awa Mtangazaji wa redio?

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...