WAKATI binti wa mwanamuziki Bobby Brown aitwaye Bobbi Kristina akiwa 'ananusa' kifo, familia yake inajadili mipango ya mazishi yake, ambapo upande wa baba yake unajizatiti kupambana kutokana na vitendo ilivyofanyiwa wakati Whitney Houston (mama yake Bobbi) alipofariki.
Kwa mujibu wa tovuti ya TMZ, familia ya Brown haitaki tena hali hiyo itokee ambapo Brown aliondoka katika mazishi hayo baada ya waangalizi wa usalama kumkataza kukaa na Bobbi wakati wa misa ya kumwombea mama yake.
Bobby ananukuliwa akisema familia ya Houston ilikasirishwa na kitendo chake cha kuja na watu tisa wa familia yake kwenye mazishi hayo.
Habari zilizopo ni kwamba chumba alimolazwa Bobbi katika hospitali akiwa mahututi baada ya kukutwa akiwa ameanguka bafuni, kimewekewa kizuizi na familia ya Houston na kuna namba maalum ya kuingilia ndani ya chumba hicho.
Wanafamilia wengi wa upande wa Brown hawakupewa namba hiyo, jambo ambalo lilisababisha kutoelewana.
"Lolote likitokea kwa Bobbi Kristina, hatutakubali kufanyiwa vitendo kama vile sisi watoto wadogo," alisema mmoja wa wanafamilia ya Brown.
0 comments:
Post a Comment