2015-02-24

MANAIKI: SIJAKATA TAMAA-------------- WALPER KAMA NILIVYO FANYA HAPA



MSANII filamu za Kibongo, Manaiki Sanga amefungukai kuwa hajakata tamaa kumuoa msanii mwenzake, Jacqueline Walper na kwamba bado anaendelea kuwashawishi wazazi wake.

Msanii filamu za Kibongo, Manaiki Sanga akiwa na msanii mwenzake, Jacqueline Walper.

Akichezesha taya na Uwazi, Manaiki aliweka wazi kuwa bado anawashawishi wazazi wake wakubaliane na uchaguzi wake kwakuwa ndiye mtu anayempenda.

“Ni upande mmoja tu wa ndugu zangu ambao wapo kijijini Mbeya na hawamfahamu Walper ila sijakata tamaa na naamini watanielewa tu kwa maaana ndoto yangu mimi ni kumuoa mtu ambaye ninampenda,” alisema Manaiki. Hivi karibuni Manaiki alitangaza nia ya kumuoa Walper ambapo wazazi wake walimkatalia na kumwambia atafute msichana wa kutoka mkoa wake.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...