Moses Machali
Mambo yaliyofanyika ni mengi na miongoni mwa mambo hayo kwanza kwa kupitia mfuko wa jimbo, nimejenga madarasa katika vijiji kama Ruhita, Nyumbigwa, Herujuu, Kalunga, Nyansha/ Nyantare, Kigondo, Kidiama na maeneo mengine.
1. Karim Manase, mkazi wa Kata ya Kumsenga.
Wilaya ya Kasulu inakabiliwa na wimbi kubwa la uhalifu na kila wanapokamatwa hata kama kuna vithibitisho vya kutosha, wahalifu hao huachwa bila kuchukuliwa hatua za kisheria na hivyo kuzidi kwa vitendo vya uhalifu.
Utafanya nini ili kukomesha tabia ya polisi kuwaachia watuhumiwa kienyeji?
Jibu: Nimechukua hatua kadhaa kulisaidia Jeshi la Polisi ili liweze kufanya kazi zao vizuri. Nimekuwa nikiwachangia mafuta na matairi ya gari ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Jibu: Nimechukua hatua kadhaa kulisaidia Jeshi la Polisi ili liweze kufanya kazi zao vizuri. Nimekuwa nikiwachangia mafuta na matairi ya gari ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Polisi kuachia wahalifu ni mwendelezo ya mambo yaleyale ya rushwa. Nimekuwa nikijadiliana na viongozi wa polisi wilaya kukomesha hali hiyo na wameniambia wanachukua hatua dhidi ya polisi wanaohusika.
Mwaka 2011, polisi wapatao tisa walifunguliwa mashtaka na kufukuzwa kazi kutokana na jitihada zangu za ufuatiliaji, yote hiyo ikiwa ni kutaka kujenga jeshi lenye nidhamu.
Wananchi wa Kasulu wanafahamu jinsi gani nilipambanania mambo haya. Changamoto ni nyingi na zinaendelea kufanyiwa kazi. Nimekuwa mtetezi wa stahiki za askari ili waweze kuishi maisha mazuri.
2. Johnson Masabo, mkazi wa Murubona.
Mwaka 2010 ulituahidi kwamba endapo utashinda utawaburuza mahakamani viongozi na watendaji wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu waliohujumu na kufuja mali na fedha ya umma. Vipi umefanikiwa?
Jibu: Ahadi yangu haikuwa moja. Nilisema nitajitahidi kuwasaidia wananchi wangu na kuisukuma Serikali kuhakikisha inafanya kazi kwa misingi ya ukweli, uwazi na uwajibikaji kwa kuwa ndiyo nguzo muhimu ya kuleta mabadiliko katika Taifa lolote lile duniani.

Hatua ambazo nimezichukua ni kuripoti kwenye mamlaka zinazostahili kuchukua hatua kwa wale wote waliofanya vitendo vya kifisadi.
Tangu nimekuwa mbunge, halmashauri mpaka leo imeongozwa na wakurugenzi wasiopungua wanne hiyo ni katika kuhakikisha kwamba kunakuwa na uwajibikaji mzuri na utendaji bora wa kazi na kukomesha ufisadi na wizi wa kila namna uliokuwa unaendelea.

Hata hivyo, ninasikitika kwamba mamlaka zinazotakiwa kuchukua hatua zimekuwa legelege kwa kufanya uhamisho usiokuwa na tija.
Nitaendelea kupambana ili kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa zaidi ya kumhamisha mtu kutoka eneo moja kwenda jingine.
3. Steven Charles, Kilamuhama mkazi wa Murubona.
Katika kipindi chote cha ubunge wako ni jambo gani la maendeleo umefanya kwa wapigakura wako ili tuwe na hamasa ya kukuchagua tena mwaka huu endapo utagombea tena?
Jibu: Mambo yaliyofanyika ni mengi na miongoni mwa mambo hayo kwanza kwa kupitia mfuko wa jimbo, nimejenga madarasa katika vijiji kama Ruhita, Nyumbigwa, Herujuu, Kalunga, Nyansha/ Nyantare, Kigondo, Kidiama na maeneo mengine.

Pia baadhi ya maeneo nimejenga vyoo vya shule na madawati ya wanafunzi na meza za walimu na viti nazo ni kama vile Shule ya Msingi Nyumbigwa, Shule ya Sekondari Nyumbigwa, pia Shule ya Msingi Mwenge, Shule ya Msingi Marumba na Kisito.
Kitu kingine ni kuanzisha miradi ya maji katika Shule ya Sekondari Muka ambayo inahudumia vijiji vya Kabanga na Msambara.
Vilevile, mradi wa kupeleka maji Kumnyika. Pia nimesaidia michezo Kasulu Mjini lakini kuna vitendo vya ufisadi vilitendeka kwa fedha nilizotoa zilitumiwa vibaya lakini sijavunjika moyo nitaendelea kuwasaidia kama watafuata ushauri na maelekezo yangu nitakayotoa.

2011 niliamua kuwalipia ada kwa fedha zangu watoto wasiopungua 60 waliomaliza msingi na kuingia sekondari ambao walifaulu lakini walitoka kwenye mazingira magumu.
Mwananchi
0 comments:
Post a Comment