2015-02-25

MONALISA, BANANA WAPATA AJALI KAZINI...............ina huzunisha sana


Staa wa filamu ya Daddy’s Wedding, Yvone Sheryl ‘Monalisa’.
MASTAA wa filamu ya Daddy’s Wedding, Yvone Sheryl ‘Monalisa’, Banana Zoro, Sandra, Mama Abdul na wenzao hivi karibuni walipata ajali walipokuwa kwenye maandalizi ya filamu hiyo kwenye mbuga ya Saadani.

Ajali hiyo ilitokea katika daraja moja dogo mbugani hapo ambapo walikusanyika kwa ajili ya kushuti mojawapo ya vipande vya filamu hiyo mpya, lakini likaporomoka na kuwafanya baadhi yao kuumia na wengine kupata mshtuko mkubwa. 

Banana Zoro. “Aliyeumia zaidi ni Sandra lakini alipewa matibabu ya haraka na kuruhusiwa, ila tunamshukuru Mungu tulifanikiwa kumaliza salama na hatukudaiwa chochote,” alisema na kumtaja pia Jenerali Ulimwengu kuwa

 mmoja kati ya waigizaji walio ndani ya filamu hiyo.
GPL

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...