2015-02-17

Ni balaaaaaaaaaa:Waigizaji wamuudhi Riyama......soma hapa kilichojiri


MWIGIZAJI wa filamu za Bongo, Riyama Ally ‘Riyama’, amesema anachukizwa na vitendo vya waigizaji kushindwa kuonyeshana upendo wa kweli.

Akizungumza jijini hivi karibuni, Riyama alisema mara nyingi amekuwa akijaribu kuonyesha upendo kwa kila msanii hata kama amemkosea.

“Ninachukizwa sana na waigizaji ambao unakuta wanagombana na kushindwa kusameheana kwa vitu vidogo,” alisema Riyama.

Alisema upande wake amekuwa muwazi na kupenda kumueleza ukweli mtu anayemkosea ili kujenga ukaribu na urafiki. 

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...