Wanafunzi ni miongoni mwa wanaoathiriwa kwa kiasi kikubwa na mashambulizi ya Taliban
Hatari ya mashambulizi ya mara kwa mara nchini Pakistani imefanya jamii ya nchini humo kuchukua hatua ambazo zimeonekana si za kawaida.
Kaskazini magharibi mwa Pakistani, Polisi wanatoa mafunzo ya namna ya kutumia silaha kwa Walimu wa shule na Chuo kikuu hatua iliyokuja baada ya Wanamgambo wa Taliban kuwaua Watu 150 katika Jimbo la Peshawar mwezi Disemba.
Wanajifunza namna ya kuweka risasi, kulenga na kufyatua.Silaha wanazotumia ni pamoja na Bastola na Bunduki, pia wanajadili kuhusu mbinu za kujilinda na namna ya kuwalinda Wanafunzi ikiwa Wanamgambo wa Taliban watavamia wakati ambapo watakuwa darasani wakisoma.
Jitihada hizi za mafunzo ya matumizi ya silaha zinatoka katika Serikali ya Jimbo la Khyber-Pakhtunkhwa na Mamlaka ya Polisi, zikiwa ni jitihada za kuimarisha usalama kwenye Shule.

0 comments:
Post a Comment